Maumbile

Bwana mmoja nchini India aliyekwenda hospitali kutokana na maumivu ya tumbo, alifanyiwa upasuaji na madaktari kukuta bwana huyo ameota kizazi cha kike.
Bwana huyo, ambaye kazi yake ni mkulima, na tayari ana watoto wawili, alitajwa kwa jina la Ryalu, na gazeti la Telegraph, ambalo limeandika taarifa hii.
Mtandao wa cnews.com umesema madaktari walidhani kuwa bwana huyo anasumbuliwa na ngiri.
Hata hivyo baada ya madaktari kumfanyia upasuaji, walikuta akiwa na viungo kamili vya uzazi vya kike.
Bwana huyo alikuwa akiishi maisha ya kawaida kabisa, huku viungo vyake vya kiume vikifanya kazi kama inavyotakiwa.
"Viungo vyake vya kiume viko sawa kabisa" amesema Daktari Pramod Kumar, akizungumza na gazeti la Telegraph. Bwana huyo ameondolewa viungo visivyo vyake, na anaendelea vizuri hospitali.
CHUKA CHINI KUTOA MAONI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.