Kujifungua mtihani

Mwanamama mmoja mja mzito nchini Marekani, alijizuia kujifungua kwa muda wa saa tatu ili amalize kufanya mtihani.
Mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 29, alianza kupata uchungu wa kujifungua muda mfupi tu baada ya kuanza mtihani wake uliodumu kwa saa tatu.
Alilazimika kuendelea kufanya mtihani huo, kwani asingemaliza mtihani wake, basi matokeo yake hayatatambuliwa.
Mwanamke huyo Nightingale Dawson wa mjini Chigago amesema alijaribu kuufanya mtihani huo kwa haraka iwezekanavyo.
Baada ya kumaliza mtihani wake, alisaidiwa na watu kupelekwa katika hospitali iliyokuwa karibu, na kufanikiwa kupata mtoto saa mbili baadaye.
Alipata mtoto wa kiume na kumuita Wilson.
"Nilijitahidi na kuvuta pumzi ndefu ili niweze kumaliza mtihani" amesema Bi Nightingale akizungumza na gazeti ta Chicago Tribune.
Matokeo ya mtihani alioufanya yatatoka wakati Wilson akiwna miezi miwii na nusu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.