MENYEKANISHA IBIKORWA VYAWE HANO

Jumamosi, 18 Januari 2014

HIVI NDIVYO MKE WA MTU ALIVYONASWA GESTI AKISUBIRI MTEJA ILI AJIUZE...MATUKIO KATIKA PICHA


blaiton news
 
Makubwa madogo yana nafuu! Kwenye kamatakamata na fumuafumua ya magenge ya biashara haramu ya ngono mjini hapa imemkumba bonge la jimama ambalo lilinaswa gesti likisubiri mteja. 
Bonge akiwa kitandani kauchapa usingizi chumbani huku kitandani kukiwa na kondomu kibao.
 
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni wakati vijana wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM)  ilipopata mwaliko maalum kutoka jeshi la polisi Moro kwa ajili ya kufichua biashara hiyo haramu ambapo mwanamke huyo alinaswa kauchapa usingizi chumbani huku kitandani kukiwa na kondomu kibao.
 
 
...bonge akiwa kitandani.
 
Ndani ya gesti maarufu ya Itigi iliyopo maeneo ya Msamvu, inayotumiwa zaidi na madereva wa malori ya masafa marefu ndipo alipobambwa bonge ambaye katika utetezi wake alidai kuwa ni mke wa mtu.
 
“Naombeni mnisamehe nilikuwa najitafutia riziki, baba J akijua ataniua jamani amesafiri, akirudi nimekwisha,” alisema kwa aibu mwanamke huyo. aliyejulikana kwa jina la mama J.
 
 
... bonge akiwa katika pozi la aibu baada ya kubanwa
 
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, kitendo hicho kilikuwa cha aibu mno mbele ya jamii.
Hata hivyo, pamoja na utetezi wake, bonge aliunganishwa na wenzake walionaswa kisha akapewa henyahenya na polisi kabla ya kutupwa nyuma ya nondo za mahabusu kusubiri sheria kuchukua mkondo wake..
ingia hapa......www.blaitontz.blogspot.com  
 
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII HAPA CHINI..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.