MENYEKANISHA IBIKORWA VYAWE HANO

Jumatatu, 7 Aprili 2014




vijana wakishikilia mwenge wa kumbukumbu, huko makao makuu ya umoja wa mataifa, New York, siku ya uzunduzi wa Kwibuka20
Miaka 20 baada ya mauaji ya kimbari, Rwanda yazidi kuimarika:
Leo tarehe 7, Aprili ni siku ya kumbukizi ya miaka 20 tangu mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon yupo mjini Kigali kushirikii kumbukizi hiyo.
Katika salamu zake Ban amesema dunia itakumbuka daima mauaji hayo, ambapo watu 800,000 walifariki dunia. Hata hivyo amewapongeza wanyarwanda kwa kuonyesha mfano wa kuungana tena baada ya vita na akitoa wito kwa viongozi kuendelea na bidii ya kuungana na kujenga nchi kwa kuheshimu haki za binadamu.
Hapa New York, Naibu Mwakilishi wa Kudumu  wa Rwanda katika Umoja wa Mataifa, Olivier Nduhungirehe, amezungumza na Idhaa hii akiangazia maudhui ya kumbukizi ya mwaka huu, ambayo ni Kumbuka, Ungana na Badilika.
Amesema ni muhimu kukumbuka waliokufa na kuendeleo kusaidia waliobaki, lakini pia kuungana ni lazima, ili kuzuia mauaji kama hayo yasitokee tena, na kubadilika ili kujenga nchi akigusia zaidi vijana ambao hawakushuhudia mauaji ya kimbari, kwani yaliyotokea Rwanda ni somo kwa dunia nzima. Balozi akasema yaliyotokea ni somo, na la kwanza ni mfumo wa kisheria.
(Sauti ya Balozi Nduhungihere)
 "Kazi kubwa sana ilifanywa na mahakama za jamii, zinazoitwa gacaca. Zilituwezesha kuhakikisha haki itendeke. Mahakama za Gacaca ziliweza kuhukuma zaidi ya watu milioni moja. Na zilikuwa ni mahakama shirikishi, ambapo wahalifu wakikiri makosa yao na kuomba radhi, walipunguzwa vifungo au adhibu zao. Kwa hiyo, tumeridhishwa sana na mafanikio ya mahakama za gacaca."
Halikadhalika akazungumzia somo la pili la jinsi Rwanda ilivyoweza kujijenga upya baada ya vita.
(Sauti ya Balozi Nduhungihere)
 " Baada ya mauaji ya kimbari, kila kitu kingeweza kutokezea. Lakini tumechagua njia ya maridhiano kati ya wanyarwanda, hata kama mauaji ya kimbari yalituathiri sana. Na hiii ni somo la muhimu sana kwa nchi nyingine zilizoshuhudia vita. Halafu tumeamua kujijenga upya na kuimarisha amani na maendeleo. Rwanda mara nyingi inatajwa kama mfano katika nchi zilizojijenga baada ya vita. Njia ya kufuatilia baada ya vita kati ya ndugu, vita iliyoharibu miondombinu yote na uchumi ndani ya nchi, ndiyo hiyo : ni kurejea kazini ili kujenga upya uchumi".  


MENGINE ZAIDIII  HAPA  Blaiton | Welcome to Blaiton News

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.