MENYEKANISHA IBIKORWA VYAWE HANO

Alhamisi, 20 Februari 2014

BUNGE NCHINI BURUNDI LIMEIDHINISHA JINA LA PROSER BAZOMBAZA KUA MAKAMU WA KWANZA RAISI WA BRUNDI

Prosper-Bazombanza

Bunge nchini Burundi limeidhinisha jina la Proser Bazombaza kuwa makamu wa kwanza wa raisi BRUNDI



post...by  blaiton.

Kikao cha wabunge mjini Bujumbura, nchini Burundi
Hatua ya kuchaguliwa kwa Prosper Bazombaza kuwa makamu wa kwanza wa rais WA BRU.     jamhuri ya Burundi na bunge nchini humo, huenda ikahatarisha zaidi mzozo wakisiasa uliopo nchini Burundi baina ya utawala wa nchi hio na chama cha 
UPRONA.

 Bazombaza ni mfuasi wa chama cha UPRONA aliependekezwa na Concilie Niragira, ambae alijitangaza hivi karibuni kua ndie kiongiozi wa chama cha UPRONA, baada ya Bonaventure Niyoyankana, ambaye alitambuliwa na seriklai ya Burundi kuwa ndie kiongozi wa chama hicho kujiuzulu.
Wabunge wa chama cha UPRONA wamepinga uteuzi wa Prosper Bazombaza kuwa makamu wa kwanza wa rais, wakisema kwamba hajapendekezwa na chama chama chao, na kubaini kwamba ni hujuma za chama tawala dhidi ya chama cha UPRONA.
Mzozo huo wa kisiasa baina ya chama tawala CNDD-FDD na mshirika wake uliibuka tangu mwishoni mwa mwezi januari, baada ya hatua ya waziri wa Mambo ya ndani Edouard Nduwimana ya kumuweka mtu wa karibu wa chama hicho Bonaventure Niyoyankana kwenye uongozi wa chama UPRONA, hatua iliyofutwa na aliekua makamu wa kwanza wa rais Bernarda Busokoza, ambaye alitimuliwa kwenye wadhifa wake.
Msemaji wa chama UPRONA Bonaventure Gasutwa amesema hizi ni hujuma za chama tawala dhidi ya chama tawala.
Upande wake naibu msemaji wa rais wa Burundi WILLY Nyamitwe, amesema kulikua umuhimu mkubwa wa kupatikana kwa makamu wa kwanza wa rais, hivo chama UPRONA kiliwasilisha wagombea na tayari makamu wa kwanza wa rais amepatikana, “vinginevyo mkanganyiko katika siasa ni jambo la kawaida”.
Kamati kuu ya chama UPRONA iliwasilisha jana kwa rais wa Burundi majina matatu ya watu, ambapo rais Pierre Nkurunziza angeliteua mtu mmoja kati ya hao kuchukua uadhifa wa makamo wa kwanza wa rais.
Majina ya watu hao yaliyowasilishwa na kamati kuu ya chama UPRONA ni Bernard Busokoza (alie makamu wa kwanza wa rais, ambaye alitimuliwa na rais Pierre Nkurunziza), Yves Sahinguvu (makamu wa kwanza wa zamani wa rais) na Thacien Sibomana.
Prosper Bazombaza aliwahi kua mkuu wa mkoa wa Mwaro (katikati mwa Burundi) katika miaka ya 2002 hadi 2005, na kabla ya uteuzi wake kwenye uadhifa wa makamu wa kwanza wa rais alikua afisa kwenye tume ya kitaifa ya kutanzua mizozo ya aridhi na milki zingine CNTB.


               TOA  MAONI  YAKO  HAPO CHINI 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.