Zaidi ya watu 50 wamefariki nchini Burundi baada ya kusombwa na maji pamoja na maporomoko ya udongo.
Kwa mujibu wa waziri wa usalama, mvua kubwa ilinyesha usiku kucha katika mji mkuu Bujumbura na kusababisha uharibifu mkubwa.
Waziri Gabriel Nizigama amesema kuwa tayari wamepata miili ya watu 50, waliofariki baada ya nyumba zao kuporomoka na kusombwa na maji.Majumba yamebomoka kufuatia mvua hiyo kubwa
Mitaa na vitongoji vya mji mkuu Bujumbura viliopo kaskazini vimeathirika zaidi.
Serikali ya Burundi mbali na kutangaza kwamba itagharamia mazishi na huduma kwa majeruhi, imetangaza pia siku moja ya maombolezi ya kitaifa siku ya Jumanne.
Miongoni mwa tarafa ambazo zimeathirika sana ni Kamenge sehemu inayopakana na mkoa wa Bujumbura. Inaarifiwa watu wengi hususan watoto wamepoteza maisha.
Majeruhi wamelazwa katika hospitali kuu za serikali mjini Bujumbura na hasa Hospital Roi Khaled.
Na kutokana na uhaba wa nafasi katika vyumba vya kuhifadhi maiti, baadhi ya maiti zimezikwa leo,kwa idhini ya familiya zao na shughuli za uokozi zinaendelea lakini zinakabiliwa na ukosefu wa vifaa, inasadikiwa kuwa maiti nyingi bado zimenaswa katika vifusi vya majumba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.