Justin Bieber akamatwa na polisi

Bieber alikamatwa Alhamisi asubuhi akiwa mlevi
Mwanamuziki mashuhuri duniani Justin Bieber,amekamatwa na
polisi nchini Marekani kwa kosa la kuendesha gari akiwa mlevi.
Polisi katika mji wa Miami Beach, wamesema kuwa mwanamuziki huyo mwenye umri
wa miaka 19 pia alikuwa anafanya mchezo wa kuendesha magari kwa kasi bila kibali
ambalo pia ni kosa.Mtandao unaofuatilia maisha ya wasanii wa kimataifa, TMZ umeripoti kuwa Justin Bieber aliondoka klabuni mapema asubuhi akiwa anaendesha gari aina ya Lamborghini wakati polisi walipomtaka kutumia kifaa
Wiki jana polisi walifanya msako katika nyumba ya mwanamuziki huyo, baada ya madai kuwa alirusha Mayai katika nyumba ya jirani yake na kusababisha uharibu wa thamani ya maelfu ya dola.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.