MENYEKANISHA IBIKORWA VYAWE HANO

Alhamisi, 23 Januari 2014

ALLY KIBA KAPATA AJALI MIKUMI MOROGORO.


Habari zilizotufikia zinasema kuwa msanii wa bongo flevaAlly Kiba amepata ajali maeneo ya Mikumi Morogoroakiwa anatokea MBEYA akiwa na steji show wake.
Nimeongea na Ally Kiba akaniambia alikuwa na show Mbeya na baada ya kumaliza show hiyo ilibidi waondoke na kurudi Dar ili aweze kupanda ndege na kuelekea Mwanzakwenye FIESTA.
Kwenye majira ya saa 11 asubuhi wakati wanakatiza Mikumi ndipo gari hilo dogo ilipopata ajali, Kiba anasema hakujua jinsi ajali hiyo ilivyotokea kwa sababu kulikuwa na giza, ila inasemekana dereva alikuwa amelala maana hakupumziki na Kiba alimwambia kama amechoka ampe yeye gari aendeshe lakini jamaa alikuwa mbishi na matokeo yake kuwa hivyo
Kiba ameumia kwenye mguu na mkono na kwa sasa yupo nyumbani kwao Dar na anaenelea vizuri.



chuka  chini  kutoa  maoni 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.