Kwa umbo lake dogo ukimuona, hutojua kama kichwa chake kimebeba uwezo wa kutosha kuushangaza umma anapokuwa na Camera mkononi. Hii ni mojawapo ya sababu iliyopelekea Mbogo Production Studios kumchukua kijana huyu ambaye kwa jina lingine anajiita Young Jay, kazi zake ni murua.
Katika mahojiano na Gospel Kitaa, Juma anaeleza kuwa ujuzi wake umeanzia mbali kutokea kwenye 'kushoot' video za mtaani wmaka 2000, kabla hajahamia kwenye harusi na sendoff, bongo fleva kabla hajaokoka, hadi pale alipokata shauri na kuanza kuleta mabadiliko kwenye tasnia ya video za injili, na hata kushoot mikutano ya injili.
Mojawapo ambayo Gospel Kitaa ikafanikiwa kuipata ni ya Raphael Segu, Yesu ni zaidi ya Kikombe cha Babu, lakini nyingine ni pamoja na ya mtoto ambaye anafanya vizuro kwenye tasnia ya muziki wa injili nchini, Miriam Chirwa na wimbo wake wa Wema wake Yesu.
Pamoja na yote, Juma anapiga picha na kuhariri (shoot & edit) filamu za Kitanzania, swali la msingi ambalo GK ilimuuliza ni; kwanini mtu aache sehemu nyingine yoyote aje kwako?
Juma; Aje JM au Mbogo kwa maana tunajali muda na kazi ataipata kwa wakati, na kiwango cha juu. Pia Mbogo Production ipo katika Promotion ambapo utapata nafasi ya kutangaziwa kazi yako kupitia kipindi cha Mbogo Studio kinachorushwa WAPO Radio FM.
Katika hatua nyingine, Juma anatoa ushauri kwa waimbaji wa muziki wa injili, "muziki wa injili sasa hivi upo juu, maana waimbaji wanazidi kumiminika kila kukicha - cha kusema ni kwamba waimbaji wawe na ushirikiano katika kazi zao, lakini na sisi pia kama 'maproduza' inabidi tuwe tunawashauri waimbaji kabla hatujawafanyia kazi zao." Anamaliza kueleza Juma Maulid katika mahojiano kwenye studio ya Mbogo Productions iliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam, mkabala na WAPO Radio FM.
Kuwasiliana na Juma moja kwa moja, unaweza kutumia mawasiliano yaliyoainishwa hapo chini, ambapo kwa kipindi hiki hadi mwezi Machi, Gospel Kitaa inakuwezesha kurekodi kwa gharama nafuu, kwa kutaja namba ya 'coupon' "GK MPV114". Changamkia kwa kadri ya uwezavyo.