Pamoja na neema inayooneka kwenye maisha ya msanii huyo, jambo lingine alilotakiwa kulitolea ufafanuzi mwanadada huyo ambaye kwa urembo ‘anaita’ ni kuporomoka kwa mwili wake na kumfanya aonekane mwembamba tofauti na zamani.
“Sielewi unaposema nimekonda unamaanisha nini, mimi naona niko vizuri, nina mwili wa kawaida, mwepesi au ulitaka niwe na minyamanyama…tehe, tehee, teheee.” Alisema Dokii na kuangua kicheko.blaiton news
Kufuatia jibu hilo, mwandishi wetu bizimen alimbana msanii huyo juu ya malipo aliyolipwa na CCM ambapo alionekana kuchemsha na kulazimika kushibisha hoja kwa kusema fedha nyingine alizipata kwenye biashara ya dawa za wanawake za kupunguza unene.
Hata hivyo, hesabu zake hazikumuingia kichwani paparazi wetu, jambo lililomlazimu Dokii kuibuka na chanzo kingine cha mapato, eti yeye ni wakala wa M-Net anayesimamia filamu za wabongo kuonekana kwenye kituo hicho cha televisheni chenye makao yake nchini Afrika Kusini.
Katika hatua nyingine, msanii huyo alishukuru kutengana na Caz T na kudai kwamba angekuwa naye mpaka leo asingepata mafanikio aliyonayo sasa.
Dokii alieleza kuwa, mbali na kununua gari hilo, pia anamiliki pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda 10 na shamba lililopo Bagamoyo, Pwani.
Dawati la Amani linampongeza mwanadada huyu kwa mafanikio aliyoyapata na kumtakia kila la kheri katika maisha yake. pata mengi www.blaiton.com
TOA MAONI HAPO CHINI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.