Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ametia saini muswada huo kuwa sheria rasmi kitu ambacho kimeibua hasira waandishi wa habari na wanahakati wa watetezi za haki za binadamu na wanahabari.
Msemaji wa Rais Nkurunziza, Leonidas Hatungimana ndiye amethibitisha hatua ya kutiwa saini kwa muswada wa sheria hiyo mpya ya vyombo vya habari kuwa sheria baada ya kuwasilishwa kwake kutoka Bungeni.
Shirika la Waandishi wa Habari wasio na Mipaka nchini Burundi wamelaani pakubwa hatua hiyo na kusema imeleta giza kubwa kwenye uhuru wa vyombo vya habari nchini humo wakisema haina lengo jema kwa wananchi na wanahabari.
Wanaharakati nao hawajakaa kimya na badala yake wamelaani vikali hatua ya kuidhinishwa kwa sheria hiyo na kusema imehalalisha kubanwa kwa uhuru wa habari nchini Burundi kwa maslahi ya watu wachache.
Umoja wa Waandishi wa Habari nchini Burundi nao umelaani vikali sheria hiyo mpya na kusema imekuja kwa lengo la kutaka kuwafunga mdomo wanahabari kuweza kufichua maovu yaliyopo.
Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Waandishi wa Habari nchini Burundi Marie-Claire Ndikumana amekiri kupokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya Rais Nkurunziza kuidhinisha muswada huo kuwa sheria mpya ya vyombo vya habari.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Radio ya African Public nchini Burundi Eric Manirakiza ameweka bayana sheria hiyo imekuja kuua uhuru wa vyombo vya habari lakini wao watendelea na mapambano.
Manirakiza ameweka bayana hawawezi kurudi nyuma kwenye mapambanoyao kwa kuwa lengo lao ni kuhakikisha demokrasia inapatikana nchini Burundi ambayo itachangia na uhuru wa vyombo vya habari.
Sheria mpya ya vyombo vya habari nchini Burundi imekuwa ikikosolewa kutokana na kuwa na vipengele vinavyowabana waandishi wa habari ikiwemo kumtaka mwanahabari kutaja chanzo chake cha habari kitu kinachokwamisha upatikanaji wa habari za uchunguzi.
Kipengele kingine kinachopigiwa kelele zaidi na wanahabari nchini Burundi ni kile kinachomtambua mwandishi wa habari ambaye atakuwa na elimu ya shahada ya kwanza na kuendelea.
Sheria hiyo ilikosolewa na vyama vyote vya siasa nchini Burundi kasoro kile cha CNDD-FDD anachotoka Rais Nkurunziza ambaye alichaguliwa tena kuongoza nchi hiyo mwaka 2013 kwenye uchaguzi uliosusiwa na wapinzani.
SHUKA CHINI KUTOA MAONI
Msemaji wa Rais Nkurunziza, Leonidas Hatungimana ndiye amethibitisha hatua ya kutiwa saini kwa muswada wa sheria hiyo mpya ya vyombo vya habari kuwa sheria baada ya kuwasilishwa kwake kutoka Bungeni.
Shirika la Waandishi wa Habari wasio na Mipaka nchini Burundi wamelaani pakubwa hatua hiyo na kusema imeleta giza kubwa kwenye uhuru wa vyombo vya habari nchini humo wakisema haina lengo jema kwa wananchi na wanahabari.
Wanaharakati nao hawajakaa kimya na badala yake wamelaani vikali hatua ya kuidhinishwa kwa sheria hiyo na kusema imehalalisha kubanwa kwa uhuru wa habari nchini Burundi kwa maslahi ya watu wachache.
Umoja wa Waandishi wa Habari nchini Burundi nao umelaani vikali sheria hiyo mpya na kusema imekuja kwa lengo la kutaka kuwafunga mdomo wanahabari kuweza kufichua maovu yaliyopo.
Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Waandishi wa Habari nchini Burundi Marie-Claire Ndikumana amekiri kupokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya Rais Nkurunziza kuidhinisha muswada huo kuwa sheria mpya ya vyombo vya habari.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Radio ya African Public nchini Burundi Eric Manirakiza ameweka bayana sheria hiyo imekuja kuua uhuru wa vyombo vya habari lakini wao watendelea na mapambano.
Manirakiza ameweka bayana hawawezi kurudi nyuma kwenye mapambano
Sheria mpya ya vyombo vya habari nchini Burundi imekuwa ikikosolewa kutokana na kuwa na vipengele vinavyowabana waandishi wa habari ikiwemo kumtaka mwanahabari kutaja chanzo chake cha habari kitu kinachokwamisha upatikanaji wa habari za uchunguzi.
Kipengele kingine kinachopigiwa kelele zaidi na wanahabari nchini Burundi ni kile kinachomtambua mwandishi wa habari ambaye atakuwa na elimu ya shahada ya kwanza na kuendelea.
Sheria hiyo ilikosolewa na vyama vyote vya siasa nchini Burundi kasoro kile cha CNDD-FDD anachotoka Rais Nkurunziza ambaye alichaguliwa tena kuongoza nchi hiyo mwaka 2013 kwenye uchaguzi uliosusiwa na wapinzani.
SHUKA CHINI KUTOA MAONI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.