MENYEKANISHA IBIKORWA VYAWE HANO

Jumatatu, 20 Januari 2014


Huyu ndio Elizabeth ‘Lulu’ Michael, na haya ndio aina ya malezi tuliyokuwa tukimpati

Kupitia kwenye vibaraza mbalimbali vya wadau wa Jukwaa Huru sanjari na wadau wangu katika kurasa zangu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, hapa ni sehemu ya mkusanyiko wa picha zenye kumuonyesha binti Elizabeth Michael, maarufu kama Lulu, na aina ya maisha ambayo tulikuwa tukimkuza kama taifa, kama wanahabari, kama wanajamii na kama Mtanzania mmoja mmoja.
Je, haya yalikuwa yanashamiri kwasababu alikuwa akiyalazimisha yeye mwenyewe au kwakuwa yalikuwa yakifanyika sisi tunashabikia kwa kuwa waandikaji, wasomaji na hata wanunuaji wazuri wa habari za skendo zenye kumhusu?
Tulimruhusu, kwa ridhaa yetu wenyewe kufanya mambo kama haya, huku tukiyashabikia ama kwa kutoa maoni yenye kuonyesha amependeza kwa mikao ya namna hii nk. Ni nani alikemea hali hizi hadharani?
Hata alipozungumza jambo ambalo halikuwa na mantiki, tulilipa uzito mkubwa sana, kuliko hata aliyelizungumza. Hatukujali ulikuwa ujinga, upumbavu, au nini. Hatukujali kuwa tunazidi kumpotosha zaidi, tulijali kumjua kwa kila hali na tukamsukuma naye kuwa anafanya kila lililokuja mbele yake, bila kufikiri maana tuliokuwa tunayapokea yenye kumhusu hatukuwa tunafikiria pia.
Mwisho wa siku, akaona kwakuwa watu wanataka kumjua kwa namna yoyote ile, basi bora auze utu wake kabisa? Na tulivyo waungwana sana, wapo wenzetu ambao walijitokeza na kumpandia dau.
Naam, huyu ndio binti yetu Elizabeth Michael, maarufu kwa jina la Lulu, ambaye hivi sasa sisi ambao tumempa makuzi ya namna hiyo hapo juu, ndio sisi ambao tunatamani mbingu zingetoboka na atumbukie kwenye tanuri la moto wa jehanam kisa “kanuua” Kanumba. Baada ya mazingira ya namna hiyo, kweli tunamtendea haki kumuombea mabaya? Na hiyo ni sehemu ndogo mno ya malezi tuliyokuwa tukimpatia.
Ninawaza kwa maandishi tu, na mawazo yangu yanaweza kuwa sawa na ya mwingine mwenye kuwaza sawa na mimi au tofauti na mtu anayewaza kinyume na mimi.
Rating: 6.7/10 (21 votes cast)
Rating: +1 (from 15 votes)
Huyu ndio Elizabeth 'Lulu' Michael, na haya ndio aina ya malezi tuliyokuwa tukimpatia 6.7 out of 10based on 21 ratings

Zenye kuhusiana na hii

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.