BINTI ambaye alikuwa akiigiza na marehemu Steven Kanumba ‘The Great’, Annifer Daud ‘Jennifer’ amefunguka kuwa anafarijika kuigiza na Philimon Lutwaz ‘Uncle D’ ambaye anampa faraja kama aliyokuwa akiipata kutoka kwa marehemu Uncle JJ.
Jennifer ambaye ameuza nyago kwenye filamu iitwayo After Death iliyoandaliwa na mwigizaji Jacqueline Wolper, mahsusi kwa kumuenzi Kanumba, alisema japokuwa muvi hiyo inamkumbusha machungu lakini anafarijika na kampani anayoipata kutoka kwa Uncle D ambaye ameigiza kama marehemu.
“Kwa kweli nimepata faraja kuigiza filamu hii ya kumuenzi marehemu Kanumba na Unlce D, amenifanya nimkumbuke Kanumba kutokana na ucheshi wake,” alisema.
“Kwa kweli nimepata faraja kuigiza filamu hii ya kumuenzi marehemu Kanumba na Unlce D, amenifanya nimkumbuke Kanumba kutokana na ucheshi wake,” alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.